Thursday, August 13, 2020

Lissu Amvaa JPM

Tundu Lissu Atakiwa Ahamie Upande wa Rais Magufuli Kutetea ...Mgombea urais kupitia tiketi ya chama cha demokrasI na maendeleo (CHADEMA) na makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ameshangazwa na kitendo cha rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijni kwao chao ndani ya miaka mitano ya uongozi wake.

Akizungumza na wananchi mkoani Simiyu aliko kwa ajili ya kutafuta wadhamini kwa ili  kugombea kwenye nafasi hiyo ya juu kabisa nchini Lissu amesema marais waliopita walipata kuongoza lakini waliheshimu ofisi na wananchi ndio maan hawakufanya maendeleo kwenye maeneo yao tu.

“Baba wa Taifa alikuwa Rais kwa miaka 24, Mzee Mwinyi miaka 10, Mzee Mkapa miaka 10 na

Jakaya Kikwete miaka 10, waliheshimu Ofisi ya Rais na wananchi, wangeweza kujenga viwanja vya ndege Vijijini kwao, miaka 5 ya Rais John Magufuli amejenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato” amesema Lissu.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/lissu-amvaa-jpm/

No comments:

Post a Comment