Sunday, August 23, 2020

Dondoo za leo; Lissu ataka kesi zake zisogezwe, Waliompiga wakamatwa na Dada yake asema ni muongo

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Tundu Lisu kutaka kesi zake zihairishwe, Dada yake Trump asema Kaka yake ni muongo na waliopiga msafara wa Lisu mawe wakamatwa. Karibu;

ZISOGEZWE MBELE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CHADEMA), Tundu Lissu amezungumzia kesi takribani sita za jinai zinazomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo moja itatajwa August 26, 2020 siku ambayo ni Uzinduzi wa Kampeni za Vyama vya Kisiasa nchini Tanzania.

“nitaenda Kisutu lakini nitaenda Kisutu baada ya kuhakikisha kwamba lile tendo la Kikatiba (Uchaguzi Mkuu) linalokuja mara moja kila baada ya miaka 5, nimelitekeleza kwa ukamilifu wake, kesi za jinai zilizopo mahakamani kama zimeweza kusimama hazijaendelea kwa miaka 3, haitashindikana kuzisogeza mbele kwa miezi miwili” – Lissu

 

DADA YAKE TRUMP ADAI NI MUONGO

Dada wa Rais Donald Trump na jaji wa zamani nchini humo amesema kaka yake ni muongo ambaye ”hana maadili”, rekodi ya siri imebaini.

Kauli hiyo ya kukosoa iliyotolewa na Maryanne Trump Barry ilirekodiwa na mpwa wake, Mary Trump, ambaye mwezi uliopita alichapa kitabu kilichomkosoa rais huyo.

”Tweet yake na uongo, oh Mungu wangu,” Bi Barry alisikika akisema. ”Ni uongo na ukatili.”

Mary Trump amesema alimrekodi shangazi yake kujikinga asiingie matatani.

Trump alijibu katika taarifa yake ailiyotolewa na Ikulu ikisema : ”Kila siku kuna jambo jipya, nani anajali.”

Rekodi hizo kwa mara ya kwanza ziliripotiwa na gazeti la The Washington Post, ambapo baadae shirika la habari la AP lilizipata.

Soma zaidi>>>

WALIOPIGA MAWE MSAFARA WAKE WAKAMATWA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linawashikilia watu 12 Wilaya ya Hai kwa mahojiano wakituhumiwa kufanya vurugu na kushambulia kwa mawe mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu alipokuwa akitafuta wadhamini.

Vurugu hizo zilitokea tarehe 14 Agosti 202  wilayani Hai ambapo zilisababisha majeruhi wanne waliojeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa hospitali ya Wilaya hiyo.

Katika vurugu hizo, baadhi ya magari yariharibika kutokana na kupondwa kwa mawe.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/24/dondoo-za-leo-lissu-ataka-kesi-zake-zisogezwe-waliompiga-wakamatwa-na-dada-yake-asema-ni-muongo/

No comments:

Post a Comment