Wednesday, August 12, 2020

Kubenea ataja sababu iliyomkimbiza asigombee Ubunge Chadema

Aliyekuwa mbunge wa Ubunge, Sued Kubenea, ametaja sababau mojawapo iliyomfanya asigombea jimbo hilo ni kutokana na migogoro iliyokuwepo kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kubenia amesema hakuwa tayari kushiriki kwenye dhambi ambayo ingesaidia jimbo hilo kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Miongoni mwa sababu iliyopelekea kutokugombea jimbo hilo tena ni kutokana na migogoro iliyokuwepo kwenye chama changu,” alisema Kubenea.

Julai 18, 2020 Kubenea aliondoka Chadema na kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/kubenea-ataja-sababu-iliyomkimbiza-asigombee-ubunge-chadema/

No comments:

Post a Comment