Tuesday, August 11, 2020

Sakata la Morrison na Yanga kujulikana leo mapema

 

Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala, amesema leo watatoa maamuzi katika mkataba wa mchezaji Bernard Morrison na Klabu ya Yanga.

Akuzungumza na waandishi wa habari jana amesema wameshindwa kufika maamuzi jana kwa sababu kuna vitu muhimu vimekosekana.

Mwanjala alisema kuna nyaraka moja ambayo ni muhimu haijapatikana, hivyo wataendelea leo na kikao chao.

“Kesi inaendelea kesho (leo) kwa ajili ya maamuzi kwa bahati mbaya hatukuweza kuyafanya kuna taarifa muhimu haijakamilika tumehakikishiwa tunaipata leo saa 2:30 asubuhi, ” alisema.

Alisema leo saa nne asubuhi wataanza kikao na maamuzi yatatangazwa na Bonifance Wambua.

“Kuweni na subira mambo yanaenda vizuri tunasubiri document upande wa Morrison haujakamilika na upande wa Yanga,” alisema Mwanjala.

Hivi karibuni mchezaji Morrison ametimkia Klabu ya Simu huku Yanga wakidai hajamaliza mkataba aliopewa wa miaka miwili.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/sakata-la-morrison-na-yanga-kujulikana-leo-mapema/

No comments:

Post a Comment