Thursday, August 20, 2020

Dondoo za leo; Chadema waahairisha mikutano ya Lisu, Makonda afunguka kukatwa, Rushwa yamponza

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Chadema kuhairisha kutafuta wadhamini kwa Lissu, Makonda afunguka kukosa uteuzi na mwisho ni juu ya Hakimu kuponzwa na rushwa. Karibu;

CHADEMA WAHAIRISHA KUTAFUTA WADHAMINI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelazimika kuahirisha zoezi la mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Mh,Tundu Lisu,kuendelea kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo taratibu za kujaza fomu kwa usahihi.

Uamuzi huo umetangazwa na mgombea wa Urais Tundu Lisu wakati wa ziara yake ya mwisho hii leo mjini Njombe huku akiomba radhi kwa wananchi wa mikoa iliyokuwa imesalia.

“Ratiba yetu ya mwanzo ilikuwa inasema baada ya mkoa wa Njombe, tungeenda Songea,Mtwara,Lindi halafu siku ya tarehe 21 Tungerudi Dar Es Salaam ili tarehe 22 twende Dodoma kuwasilisha fomu za uteuzi wa Rais na Makamu wa Rais”alisema Lisu

MAKONDA AFUNGUKA KUKOSA UTEUZI

Baada ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza wateule wa nafasi za Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 huku jina la Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam likikatwa.Muda mchache baada ya zoezi hilo kumalizika ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hata kama maombi yake hayajajibiwa, atabaki kumwamini Mungu wake

Kwenye kurasa yake yenye jina baba_keagan (MSTAAFU) aliandika“Nina mwabudu Mungu aliye hai. Hata asipo jibu sawa na maombi yangu, bado atabaki kuwa Mungu wangu”

Soma zaidi>>>

RUSHWA YAMPONZA HAKIMU

Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Magugu Ndugu Adeltus Richard Rweyendera, amefikishwa mahakamani na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara kwa kosa la kuomba  na kupokea rushwa ya shilingi 150,000.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kaimu mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Isdory Kyando amesema mtuhumiwa huyo alipokea rushwa hiyo kutoka kwa wazazi na ndugu wa washtakiwa wanne ambao walikuwa wanashtakiwa kwenye kesi namba 242/2020 ikiwa ni kishawishi cha kuwasaidia na kuwaachia washtakiwa hao kwenye kesi tajwa ambayo alikuwa anaisikiliza.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/21/dondoo-za-leo-chadema-waahairisha-mikutano-ya-lissu-makonda-afunguka-kukatwa-rushwa-yamponza/

No comments:

Post a Comment