Inaki Williams ni kati ya wachezai sita wa Bilbao walioambukzwa COVID19. Picha: Hisani
Inaki Williams alitangaza kupitia kwa ukurasa wake wa kijamii kuhusu kuambukizwa COVID19
Ripoti imebaini kuwa jumla ya wachezaji sita wa klabu hiyo wameambukizwa corona
Nyota wa Athletico Bilbao Inaki William amejitokeza wazi na kutangaza kuwa alipatikana na virusi hatari vya corona baada ya awamu ya pili ya vipimo kufanyiwa timu hiyo.
Matokeo hayo yaliyotolewa na PCR baada ya kupimwa wachezaji, makocha na manaibu wao yamebainika kuwa takriban watu sita katika klabu hiyo wanaugua virusi vya corona.
Ingawa klabu hiyo haijatoa habari rasmi kuhusu walioambukizwa corona katika timu hiyo, Inaki Williams kupitia kwa ukurasa wake wa kijamii amebaini kuwa ameambukizwa.
‘’ Walithibitisha kupitia vipimo vya PRC kuwa nilipatikana na virusi vya corona. Sionyeshi dalili zozote na hali yangu ipo shwari. Ni wakati wa kukaa nyumbani karantini hadi nipone. Natamani sana kujiunga na timu tena kwa maandalizi,’’ aliandika katika ukurasa wa twitter.
Haya yanajiri saa 24 tu baada ya klabu ya Barcelona kutangaza kuwa mmoja alipatikana na virusi vya corona kati ya tisa waliopimwa.
Hata hivyo Barcelona imebaini kuwa mchezaji anayeugua si mmoja kati ya timu inayotarajia kuchuana naBayern Munich katika robo fainali ya ligi ya mabingwa Ijumaaa, Agosti 14.
Klabu zingine zilizoathiriwa na virusi vya corona ni Valencia na Atletico.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/nyota-wa-athletico-bilbao-athibitisha-anaugua-covid19/
No comments:
Post a Comment