Sunday, August 16, 2020

Dondoo za leo: Watakaokatwa CCM kujulikana wiki hii, Mwenyekiti mbaroni kwa tuhuma rushwa ya ngono na Nape arusha kijembe

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Jumatatu ya Agosti 17, 2020.

Habari hizo ni Hatma ya wagombea Ubunge kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujulikana wiki hii, Mwenyekiti mbaroni kwa tuhuma rushwa ya ngono na Nape arusha kijembe.

Karibu msomaji wetu:

WATAKAOKATWA CCM KUJULIKANA WIKI HII

MAJINA ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaoteuliwa kugombes ubunge kwenye Bunge la Tanzania na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar yanatarajiwa kufahamika wiki.

CCM imetoa ratiba ya vikao vya uteuzi wa wabunge na wawakilishi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, vikao hivyo vya kuchekecha majina vinaanza leo. Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitaketi kesho na pia kitafanyika kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa.

Agosti 20 hadi 21 kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Agosti 22 Jumamosi kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Soma zaidi

MWENYEKITI MBARONI KWA RUSHWA YA NGONO

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, inamshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimana, Wilson Ngolanya (63), kwa tuhuma za rushwa ya ngono.

Taarifa za kukamatwa kwa mwenyekiti huyo zilitolewa jana na Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa, Holle Makungu, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema Ngolanya alikamatwa Agosti 15, majira ya jioni katika nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Kibaya akiwa utupu huku akiwa amevalia kondomu tayari kwa kutekeleza uhalifu huo.

Soma zaidi

NAPE ARUSHA KIJEMBE GIZANI

Mgombea ubunge jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema  uchaguzi unapomalizika wakubwa hukutana na kumaliza tabu inabaki kwa wapambe.

Nape ameandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa twitter kuwa “Naangalia makamiano kuelekea uchaguzi wa Oktoba 28 … kwa hulka ya wanasiasa uchaguzi ukiisha wakubwa hukaa na kumaliza, tabu hubaki kwa wapambe sasa ambao leo wanakesha karibu kuchomoka roho,”

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/dondoo-za-leo-watakaokatwa-ccm-kujulikana-wiki-hii-mwenyekiti-mbaroni-kwa-tuhuma-rushwa-ya-ngono-na-nape-arusha-kijembe/

No comments:

Post a Comment