Tuesday, August 11, 2020

Maafisa Watano Wakamatwa Kwa Kuiba Pombe Katika Mkasa wa Ajali

Picha ya afisa wa polis akikamatwa. Picha: Hisani

Maafisa hao waliachwa kulinda lori la kusafirisha pombe baada ya lori hilo kubingiria

Maafisa hao waliuzuia umma uliotaka kupora pombe hizo huku wao wakichukua nafasi ya kujiburudisisha kwa vileo hivyo

Kando na kubugugia pombe hiyo, maafisa hao walibeba chupa kadhaa za pombe hiyo hadi katika nyumba zao

Maafisa watano wa polisi wamekamatwa na kuzuiliwa Kisumu baada ya kuiba pombe kutoka kwa lori.

Judgement on the Computer Misuse and Cybercrimes Law to be Passed ...

Kulingana na kisa hicho kilichofanyika Jumatatu, Agosti 10, maafisa hao wanne wa kituo cha polisi cha Boya, kaunti ya Kisumu wakiongozwa na OCS William Cheruiyot wanatarajiwa kufikishwa kortni baada ya kuiba pombe kutoka kwa lori moja iliyoanguka barabarani.

Maafisa hao waliowekwa kulilinda lori hilo la pombe lisiporwe walichukua hatua ya kubugia pombe kabla kuchukua chupa zingine na za kileo hicho na kuweka katika majumba yao.

Badala ya kufanya kazi ya ulinzi, waliiba pombe kutoka kwenye lori hilo, zaidi ya chupa 72 zikinaswa kwao.

Katika ripoti iliyoonwa na Bongo Leo, kiongozi wa kituo hicho cha Boya alizuiliwa katika kituo cha Kisumu Central huku uchunguzi kuhusu kisa hicho kikiendelea.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/maafisa-watano-wakamatwa-kwa-kuiba-pombe-katika-mkasa-wa-ajali/

No comments:

Post a Comment