Thursday, August 13, 2020

Mhadhiri wa Udom aliyetaka ngono kwa mwanafunzi wake afunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma inatarajia kumfikisha mahakamani Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jacob Nyangusi (43) na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kinyume cha sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11/2007.

Mkuu wa Takukuru Dodoma, Sosthenes Kibwengo, aliyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema watamfikisha mahakamani leo jijini Dodoma.

Alisema majira ya saa 3 usiku Oktoba 3, 2018 Takukuru ilimkamata Nyangusi  akiwa nyumbani kwake eneo la nyumba mia tatu jijini Dodoma muda mfupi kabla hajatekeleza nia ovu ya kufanya ngono na aliyekuwa mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza wa shahada ya Sanaa katika Jiografia na Mazingira.

Alisema awali alipokea taarifa kuwa mtuhumiwa alimtaka mwanafunzi wake kingono kama sharti la kumsaidia ili aweze kufanya mitihani ya marudio na kumuwezesha kufauli katika somo lake.

“Ndipo tukaweka mtego kumkamata baada ya uchunguzi kukamilika na Ofisi ya Mashtaka kuridhia kwa mujibu wa sheria ndipo mtuhumiwa anafikishwa mahakamani,” alisemaKibwengo



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/mhadhiri-wa-udom-aliyetaka-ngono-kwa-mwanafunzi-wake-afunguliwa-kesi-ya-uhujumu-uchumi/

No comments:

Post a Comment