Wednesday, August 12, 2020

Fatma Karume: Limetokea Tetemeko siwezi kukaa kimya kisa Abbas katunga kanuni za kusema sina ruksa

Wakili wa kujitegemea, Fatuma Karume, amesema hawezi kukaa kimya anaposikia habari kama vile kuna tetemeko aache kuwajulisha umma.

“Eti nihisi kuna tetemeko la ardhi niogope kuujulisha umma kwa sababu Abbas katunga kanuni za kusema sina ruksa,” aliandika Fatma ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter

Alisema endapo akifanya hivyo atakuwa mpumbavu na atakuwa amekosa ubinadamu.

“Kwenye dharura eti nikae kimya kwa kumuogopa Abbasi? hata ubinadamu wameusahau?,” alihoji Fatma

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/fatma-karume-limetokea-tetemeko-siwezi-kukaa-kimya-kisa-abbas-katunga-kanuni-za-kusema-sina-ruksa/

No comments:

Post a Comment