Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema amekuwa akipokea taarifa nyingi za vitisho vya kifo tangu juzi (Jumapili) na kuwataka Wanachama kuwasindikiza wagombea Ubunge na Udiwani NEC kuchukua fomu.
Akizungumza na wakazi wa mkoa wa Singida ambako yupo kwa nia ya kitafuta wadhamini kabla ya kurejesha fomu za kugo,nea urais kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi Oktoba Lissu amesema sasa sio muda wa kutishana na wajibu wa vyombo vya usalama kuwalinda watu wote.
“Katika mazingira ya kawaida ningeweza kusema hivi ni vitisho tu, lakini hatuishi tena katika mazingira ya kawaida. Tangu Septemba 07, 2017 na yale marisasi yote yale hatuwezi tukapuuzia tena kitisho chochote, Huu sio muda wa kutishana tena, huu ni muda wa Uchaguzi wananchi wa Tanzania wapate viongozi wanaostahili” amesema.
Lissu ameeleza kuwa jukumu na wajibu wa kisheria wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha wanaopanga mipango ya mauaji wanachukuliwa hatua zinazostahili.
CHANZO: JAMIIFORUMS
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/tundu-lissu-adai-kupokea-vitisho-vya-kuwawa/
No comments:
Post a Comment