Friday, August 21, 2020

Dondoo za leo; Chenge nimefurahi sana kukatwa, Amfuata Membe ACT Wazalendo, Kuchukua fomu leo

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Chenge afunguka kukatwa, amfuata Membe na mwisho ni juu ya Katambi kuchukua fomu leo Shinyanga.

Karibu;

CHENGE, MWAKYEMBE WAFUNGUKA KUKATWA

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza majina ya wanachama wake walioteuliwa kupeperusha bendera kwenye kinyang’anyiro cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vigogo waliokatwa wametoa ya moyoni kuhusu uamuzi uliofanywa dhidi yao.

Wakizungumza jana katika mahojiano maalum na Nipashe, baadhi ya wanachama hao ambao wengine walikuwa mawaziri na wabunge wazoefu, walisema wamekubaliana na uamuzi uliofanywa na vikao vya juu vya chama.

ANDREW CHENGE

Aliyekuwa Mbunge wa Bariadi mkoani Simiyu, Andrew Chenge, ambaye aliongoza kura za maoni katika jimbo hilo, alipoulizwa kuhusu uamuzi uliofanywa dhidi yake, alijibu kwa kifupi kwamba amefurahi sana.

“Nimefurahi sana,” alijibu Chenge ambaye amekuwa mbunge kwa kipindi kirefu na kutoa mchango mkubwa katika utungaji wa sheria na uandaaji wa bajeti ya serikali.

Nipashe pia iliuliza Chenge kama yuko tayari kushiriki kampeni kukisaidia chama kupata ushindi na akatoa jibu lilelile kwamba amefurahi sana.

Soma zaidi>>>

AMFUATA MEMBE ACT

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini mwaka 2010 mpaka 2015 kupitia CCM, Dk David Malole leo amechukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

Katika Jimbo la Tunduru, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru na baadaye Tunduru Kusini kwa tiketi ya CCM 2007-2015 Mtutura Abdallah Mtutura amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na ACT Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo,  Ado Shaibu katika Ofisi ya ACT Wazalendo Tunduru.

Soma zaidi>>>

KUCHUKUA FOMU LEO

Mgombea wa Nafasi Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi (CCM) amewasili mkoani Shinyanga ambapo leo Jumamosi Agosti 22,2020 atachukua Fomu ya Kugombea Ubunge kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini tayari kwa kuanza rasmi mchakato wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020. 
Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Said Bwanga amesema Katambi ambaye ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC) kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, atachukua Fomu kesho majira ya saa tatu asubuhi katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini.


source http://www.bongoleo.com/2020/08/22/dondoo-za-leo-chenge-nimefurahi-sana-kukatwa-amfuata-membe-act-wazalendo-kuchukua-fomu-leo/

No comments:

Post a Comment