Mgombea bunge wa jimbo iringa mjini (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa ameandikia barua tume ya uchaguzi nchini juu ya kutokuwa na imani na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi kwenye jimbo la Iringa mjini kutokana na vitendo vyao kuonyesha ukada wao kwa chama cha mapinduzi (CCM).
Akizungumza na kituo cha redio cha East Afrika, Msigwa amesema wameandika barua huyo kwakua wanataka uchaguzi uwe huru na haki huku wakitaka kusiwe na figisu za aina yoyote kutokana na mapenzi yao kwa nchi.
“Tumemwandikia barua Mkurugenzi kwamba kuna baadhi ya wasimamizi hatuna imani nao kabisa kwa kuwa wameonesha ukada wa CCM, tungetaka watu wengi, tunaamini kwamba figisu zitafanywa lakini sisi tungependa uchaguzi ulio huru na wenye haki kwa sababu tunaipenda nchi yetu” amesema Msingwa.
Msigwa amejitokeza leo kwenye ofisi za tume ya uchaguzi nchini kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa chama cha Chadema zoezi lilifunguliwa leo na NEC.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/msigwa-atuma-ujumbe-nec/
No comments:
Post a Comment