Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mshambuliaji mpya aliyejiunga na timu hiyo kutokea Yanga, Bernard Morrison ni mtu muungwana na timu yake ya zamani ilikuwa inamtengenezea zengwe tu aonekanae mtu mbaya mbele ya jamii.
Katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa instrgram amesema,wanasimba watampa kila aina ya ushirikiano Morrison kwakaua wanajua atawalipa wema kutokana na wema ambao ametendewa na klabu hiyo.
“Moyo umetulia sasa, Vita yako ilikuwa yetu, Wanasimba wanakuamini utalipa wema kwa wema kwa kujituma na kujitoa kwa ajili ya klabu yetu, Nikuhakikishie Wanasimba watakupa full support ili uwaprove wewe sio mkorofi, Nimekaa na ww siku chache tu, nimekuona ni mtu Muungwana na mkweli, mengine ni Uto tu walikuwa wanakutengenezea drama tu” ameandika Manara.
Kwa kipindi kirefu kilichopiata morrison aliingia kwenye mgogoro mara kadhaa na waajili wake wa zamani timu ya Yanga na mara ya mwisho alidaiwa kukamatwa na jeshi la polisi kutokana na kubishana na polisi.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/alichokisema-manara-baada-ya-morrison-kutua-kambini-simba/
No comments:
Post a Comment