Wednesday, August 12, 2020

COVID19 Yarejea New Zealand kwa Kishindo Baada ya Miezi Mitatu Bila Maambukizi

New Zealand PM Ardern calls September election

New Zealand Yarekodi visa Vinne Vya Maambukizi ya COVID19 baada ya Miezi 3 Bila Maambukizi. Picha:Hisani.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo alithibitisha kuhusu visa vinne vya maambukizi mapya

Ametoa amri ya kufungwa shule kwa siku tatu na kusitisha mikutano ya zaidi ya watu kumi

Maambukizi ya virusi hatari vya corona vimerejea nchini New Zealand kwa mara nyingine baada ya siku 102 bila maambukizi yoyote.

Habari kuhusu mambukizi hayo mapya yalitangazwa na Waziri mkuu Jacinda Ardern.

Akitangaza kuhusu visa vinne vipya vyaa maambukizi, Jacinda alifunga shule kwa siku tatu na kusitisha mikutano ya zadi ya watu kumi kama njia ya kupambana na hali hiyo.

Aidha, alieleza kuwa masharti hayo yataanza Jumatano, Agosti 12

‘’ Kuhusiana na masharti yetu, tunawaomba wakazi wa Auckland kuchukua hatua upesi, kuanzia adhuhuri ya Jumatano, Agosti 12,tutaongeza masharti zadi,’’ Ardern alisema.

Kulingana na masharti hayo mapya, baadhi ya biashara kama vile mahoteli, mabaa na zile zisizo muhimu zaidi zitafungwa.

Mkurugenzi wa afya nchini humo Ashley Bloomfiel alibaini kuwa kati ya wanne walioripotiwa kuambukizwa virusi hivyo, hakuna aliye na historia ya usafiri wa nje ya nchi.

‘’ Tumekuwa tukijiandaa kwa wakati huu, na umefika. Idara ya afya imejitayarisha ipasavyo,’’ Bloomfield alinukuliwa na jarida la CNN.

Virusi hivyo vimerejea nchini humo baada ya nchi hiyo kusherehekea siku 100 bila maambukizi.

New Zealand records three new coronavirus cases ahead of decision ...

Wahudumu wa afya wa kupambana na COVID19. Picha: Hisani.

New Zealand imepongezwa pakubwa katika hatua iliyochukua katika kujikinga na virusi hivyo.

Humu nchini hakuna visa vya maambukizi yoyote iliyoripotiwa kwa miezi mitatu, serikali ikitangaza kuwa virusi hivyo vimepigwa teke kwa uwezo wa Mwenye Mungu.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/covid19-yarejea-new-zealand-baada-ya-miezi-mitatu-bila-maambukizi/

No comments:

Post a Comment