Wednesday, August 12, 2020

Marehemu aliyezikwa mwaka mmoja uliopita adaiwa kuonekana mtaani, polisi wafukua kaburi

Jeshi la polisi mkoa wa Geita limelazimika kufukua kaburi eneo la Nyamitogo la mtu anayedaiwa kufariki mwaka mmoja uliopita kisha kuonekana mtaani na kuzua taharuki kwa wananchi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mtatiro Kitinkwi alisema ndugu wa marehemu huyo walifika kituoni wakiwa na mtu aliyefananishwa na marehemu.

“Sisi kama jeshi la polisi tulifanya uchunguzi na moja ya uchunguzi huo ni lazima tujiridhishe kwenye kaburi alilokuwa amezikwa marehemu huyo aliyezikwa Novemba 26, 2019.

Alisema walikuta mabaki ya marehemu wakaona hilo jambo halina ukweli wowote zaidi ya kuzua taharuki.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/marehemu-aliyezikwa-mwaka-mmoja-uliopita-adaiwa-kuonekana-mtaani-polisi-wafukua-kaburi/

No comments:

Post a Comment