Tuesday, August 11, 2020

NEC Yatoa Ufafanuzi Mgombea Huru

Naomba kufahamishwa wasifu wa Dkt. Wilson Mahera, Mkurugenzi mpya ...Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya uchaguzi (NEC) Dkt.Willson Mahera amesema tume hiyo haitaruhusu mgobea binafsi kuchukua fomu ya kugombea urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.

Akizunguzma na wanahabari jijini Dodoma Dkt.Mahera amesema tume hiyo inafanya kazi kwa kuangalia sheria za uchaguzi kwa unagalizi wa katiba ya nchi ambayo hairuhusu mgombea binafsi kugombea kwenye uchaguzi wowote wa nchini.

“Tume ya taifa ya uchaguzi inafanya kazi kwa kutumia sheria na kwa kufuata katiba ya Tanzania na kama mnavyojua sifa za Rais zipo wazi na zinaeleweka na ni lazima awe mtanzania wa kuzaliwa na awe ana miaka kwanzia 40 na kundelea na lazima awe ametoka kwenye chama cha siasa” amesema Dkt Mahera.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/nec-yatoa-ufafanuzi-mgombea-huru/

No comments:

Post a Comment