Thursday, August 27, 2020

Dondoo za leo; Lissu kuwasha moto leo, Akutwa na Corona, Wagombea 57 Chadema waenguliwa walia

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja ni Lissu kukiwasha Mbagala leo, Pogba akutwa na Corona na mwisho ni juu ya wagombea 57 wa Chadema kuenguliwa. Karibu;

LISSU KUWASHA MOTO LEO

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, atazindua kampeni zake za uchaguzi mkuu kesho Ijumaa 28 Agosti 2020 jijini Dar es Salaam.

Ratiba iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema inaonyesha Lissu na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu watatumia siku tatu jijini Dar es Salaam.

Wakati Chadema wakizinduliwa kampeni zao Dar es Salaam, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli yeye anazinduliwa kampeni Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020.

Soma zaidi>>>

AKUTWA NA CORONA

PAUL Pogba, kiungo wa Manchester United, ameachwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa, baada ya kubainika kuambukizwa virusi vya corona (COVID-19).

Kikosi hicho cha Ufaransa kitacheza michezo miwili ya kirafiki na Sweden tarehe 5 Septemba 2020 na mchezo wa pili kitacheza nyumbani Paris 8 Septemba 2020.

Mchezaji mwingine ambaye ameachwa katika kikosi hicho baada ya kukutwa na  corona ni kiungo wa Tanguy Ndombele wa timu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza.

Soma zaidi>>>

WAGOMBEA WAO 57 WAENGULIWA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai wagombea wake 57 wa nafasi za ubunge na 600 wa udiwani wameshaenguliwa, kikiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua hatua stahiki.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA), Benson Kigaila, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mwenendo wa wagombea wa chama hicho. PICHA: JUMANNE JUMA

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, aliitaka NEC kuwafuta kazi wasimamizi wa uchaguzi katika baadhi ya majimbo na kata zilizoonekana kuwa na kikwazo hicho na kuwarejesha wagombea wao walioenguliwa.

Benson Kigaila alisema kuwa iwapo tume haitafanya hivyo, chama hicho kitatangaza msimamo wao na kuongeza kuwa ni muhimu kwa tume kulinda haki za wagombea wote bila upendeleo.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangalie kidogo dhana hii ya watu wanaomba msaada / kupendwa kusaidiwa wao huwa wagumu kutoa msaada.

Mdau katika mtandao anasema haelewi kwanini watu wengine wako hivi lakini kwa utafiti mdogo alioufanya amegundua asilimia kubwa ya watu wanaopenda kusaidiwa wakiwa na shida wao huwa na roho ngumu katika kusaidia wenzao wanapokuwa na shida

Anasema watu wa aina hii wakiwa na shida huwa wanaongoza kuwalalamikia na kuwasema vibaya watu ambao wanawaona wana uwezo ila wanashindwa kuwasaidia lakini wao wakipata baada ya kusaidiwa wanabadilika na kusahau wema waliotendewa

Je, unakubaliana au kupingana na mawazo ya mdau kwa kiwango gani?



source http://www.bongoleo.com/2020/08/28/dondoo-za-leo-lissu-kuwasha-moto-leo-akutwa-na-corona-wagombea-57-chadema-waenguliwa-walia/

No comments:

Post a Comment