Mamlaka ya hali ya hewa Tanazania (TMA), imesema hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko lililoteke jana kwa baadhi ya mikoa.
Jana saa 2:14 majira ya usiku tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcher 5.9 katika eneo la kusini Mashariki mwa mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi lililotokea.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA imeeleza wamefanya uchambuzi katika kituo chake cha tahadhari ya Tsunami ili kuona na kujiridhisha kwamba kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini.
“Tetemeko hilo halikuwa na nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha Tsunami”-Imeeleza taarifa hiyo.
TMA imewatoa hofu watumiaji wa eneo la bahari pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli zao kwa kuzingatia taarifa zinazo tolewa na mamlaka hiyo.
Hata hivyo TMA imesema kutokana na tetemeko hilo hakuna athari iliyojitokeza au inayotarajiwa kujitokeza katika mifumo ya hali ya hewa ya bahari.
TMA imeeleza inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa baharini na kutoa taarifa endapo kutajitokeza mwenendo wa matetemeko katika eneo la bahari.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/tma-imesema-hakuna-tishio-la-tsunami-kutokana-na-tetemeko-lililotokea/
No comments:
Post a Comment