Monday, August 10, 2020

Dondoo za leo: Mbaroni kwa kumchinja mtoto wa kambo na kufariki, MR Kuku anaswa kwa kuchezesha upato wa mabilioni ya fedha na Zahera kurejea nchini asaini mkataba

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Agosti 11, 2020.

Habari hizo ni Ayoub John anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumchinja mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu na kufariki dunia kulikoni?, MR Kuku amefikishwa mahakamani kwa kuchezesha upatu wa mabilioni ya fedha na Aliyekuwa kocha wa Klabu ya Yanga Mwinyi Zahera kurejea nchini je unajua amesaini mkataba kwa timu ipi? Soma habari hizo kwa kina.

Karibu msomaji wetu:

MBARONI TUHUMA KUUA MTOTO WA KAMBO

JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Ayoub John (38), mvuvi katika kisiwa cha Chakazimbwe wilayani Muleba kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja mtoto wake wa kambo Aidan Greyson (3).

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema jana kuwa mtoto huyo wa kiume anadaiwa kuuawa na baba yake wa kambo usiku wa kuamkia Agosti 8, mwaka huu.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi baina ya John na mke wake ambaye ni mama wa mtoto huyo, Mektirida Nestory (27). Kutokana na ugomvi huo, alisema Nestory alikimbia kwa kuhofia maisha yake na kumwacha mtoto ndani ya nyumba.

Soma zaidi

MR KUKU ANASWA KWA KUCHEZESHA UPATO WA MABILIONI YA FEDHA

 

Mfanyabiashra na Mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Tariq Machibya miaka (29) maarufu Mr Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake leo Agosti 10,2020 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Wankyo amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 60/2020 ambapo katika mashtaka hayo saba yanayomkabili mshtakiwa huyo, yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu; kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila kuwa na leseni na mashtaka matano ni kutakatisha fedha.

Soma zaidi

ZAHERA KUREJEA NCHINI ASAINI MKATABA

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amesaini mkataba wa kufundisha klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda kucheza ligi kuu kuanzia msimu ujao.

Zahera aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instragram majira ya usiku kuwa anarudi Tanzania kuungana na timu ya Gwambina ambayo itacheza ligi Kuu Tanzania bara Agosti 21, 2020.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/dondoo-za-leo-mbaroni-kwa-kumchinja-mtoto-wa-kambo-na-kufariki-mr-kuku-anaswa-kwa-kuchezesha-upato-wa-mabilioni-ya-fedha-na-zahera-kurejea-nchini-asaini-mkataba/

No comments:

Post a Comment