Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametoa shuruhisho kwa shirikisho la soka nchini juu ya sakata linaloendelea kwenye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji la shirikisho hilo kati ya mchezaji Bernard Morrison na klabu yake ya Yanga.
Manara ametoa suluhisho hilo kwenye ujumbe huo alituma kwenye mtandao wa Instagram saa chache kabla ya mwenyekiti wa kamati hiyo kutoa muongozo juu ya kilichochangia kikoa hicho kutoa majibu kwa haraka.
“Kama suala la *MORRISON* limekuwa gumu kwa TFF bac ipigwe game moja kati ya SIMBA na YANGA atakayeshinda ndo amchukue Morrison Mbona simple tu” ameandika Manara.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/manara-atoa-suruhisho-sakata-la-morrison/
No comments:
Post a Comment