Wednesday, August 12, 2020

Tetemeko la ardhi lapita mikoani ikiwemo Dar es Salaam, Wahindi wahaha Posta

Tetemeko ardhi  limeripotiwa kutokea jijini Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Arusha muda mfupi uliopita na kuibua sitofahamu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotufikia hadi sasa hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa.

Mjiolojia Gabriel Mbogoni amesema mpaka sasa bado hawajasoma kwenye mfumo kujua ni la kiwango gani.

Tetemiko hilo zimezua hekaheka kwa wananchi huku ikiekezwa kwa kuwa wahindi wanaoishi eneo la Posta walitoka huku wakiogopa kurudi katika nyumba zao.

Katika eneo la Mwenge kwa wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha Tumaini (Tudarco) baadhi wanadaiwa kuzimia kutokana na hekaheka za tetemeko.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/tetemeko-la-ardhi-lapita-mikoani-ikiwemo-dar-es-salaam/

No comments:

Post a Comment