Wednesday, August 12, 2020

Arsenal Mbioni Kuwauza Wachezaji Watatu kumsaini Nyota wa Atletico

Thomas Partey Cools Atletico Exit Talk Amid Manchester United ...

Thomas Partey. Picha: Hisani

Mirkel Arteta anatazamia kumsaini Thomas Partey kuimarisha timu yake

Arsenal inadaiwa kuwa tayari kupeana Bellerin ,Lacazette na Torreira na kuongzea hela zaidi kumkwachua mshambulizi huyo

Artletico inatarajia kumuuza nyota huyo kwa kima cha £45 milioni

Klabu ya Arsenal imechukua hatua ya kuwanadi wachezaji wake watatu na fedha zaidi kwa klabu ya Atletico ili kumsaini nyota wa klabu hiyo Thomas Partey.

Inadaiwa kuwa wachezaji watatu ambao Arsenal inatarajia kupena kwa Artletico ni Hector Bellerin, Lucas Torreira na Alexandre.

Mikel Arteta anaamini kuwa hatua ya kumsaini mshambulizi huyo itaipa timu yake makali zaidi na kumwezesha kuzoa vikombe zaidi msimu ujao.

Thomas Partey, Atletico Madrid star, reportedly emerges as target for Arsenal

Licha ya kuwa na timu iliyoonekana kuwa dhaifu msimu jana,  Arteta aliweza kufuzi kushiriki Uropa baada ya kuibuka mshindi wa FA.

Kocha huyo anaamini kuwa raia huyo wa Ghana ataimarisha nguvu zaidi katika kiongo cha ushambulizi na hivyo yuko tayari kuwaondoa wachezaji watatu kwa ajili yake.

Arsenal italazimika kuwapa Atletico wachezaj hao watatu pamoja na hela zaidi baada ya kufeli kufika bei ya £45 milioni ambayo klabu hiyo inahitaji kumuuza Partey.

Kwa uapnde mwingine, Atletico pia inadaiwa kumwinda Lacazette.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/arsenal-mbioni-kuwauza-wachezaji-watatu-kumsaini-nyota-wa-atletico/

No comments:

Post a Comment