Sunday, August 16, 2020

Mchomvu Atuma Ujumbe Mzito Kwa Mbasha

EXCLUSIVE: ADAM MCHOMVU ATANGAZA KUACHA KAZI! | "NILIPASUANA NA ...Mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha Clouds Fm, Adam Mchomvu amemuomba msamaha muimbaji wa nyimbo za injili na muhubiri Emmanuel Mbasha baada ya kitendo chake cha mpiga kwenye tamasha la kutambulisha nyimbo za chama cha mapinduzi (CCM).

Adam ameomba msahama kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram, baada ya kupokea simu za viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha mapinduzi (CCM) juu ya swala hilo.

“Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha Mimi sina tatizo lolote binafsi na Wewe kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania. Sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa” andika Mchomvu.

 

View this post on Instagram

#Ameandika @adamchomvu Dear #WashkajiZangu kwanza nimuombe radhi Rais wetu wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Pili kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuniamini na kunipa nafasi ambayo bahati mbaya ilitokea tukapishana kauli jukwaani na bwana ndugu Msanii mwenzangu. Nimepokea simu mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakinifahamisha namna nilipaswa kufanya wakati wa shambulio lile la mimi kuitwa 'ADAM Unajua we ni Bangi sana' Kwa pamoja nimewaelewa. . . Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha Mimi sina tatizo lolote binafsi na Wewe kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania. Sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa… 🇹🇿

A post shared by Clouds FM🇹🇿 (@cloudsfmtz) on



source http://www.bongoleo.com/2020/08/16/mchomvu-atuma-ujumbe-mzito-kwa-mbasha/

No comments:

Post a Comment