Friday, August 14, 2020

Sugu: Nimeachiwa na polisi bila chaji najiuliza ni kweli walitaka kupora fomu?

Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu amesema wamemuweka ndani kwa masaa matatu na kuachiwa bila chaji.

Sugu amesema amepandishwa karandinga na kuwekwa selo na wanambeya 15 akiwemo bibi wa miaka 70.

“Baada ya masaa matatu wametuachia bila chaji yoyote! Tunajiuliza what was the Motive? Ni kweli walitaka kupora fomu?,” alihoji sugu katika ukurasa wake wa twitter.

Sugu alikamatwa jana na wafuasia wa Chadema 15 baada ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge kwa madai kuwa amefanya maandamano kinyume cha sheria.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/15/sugu-nimeachiwa-polisi-bila-chaji-najiuliza-ni-kweli-walitaka-kupora-fomu/

No comments:

Post a Comment