Friday, August 7, 2020

Pigo kwa Real Madrid, Gareth Bale Adinda Kucheza Dhidi ya Manchester City

Gareth Bale lifts the lid on his Tottenham exit, his future ...

Gareth Bale ameamua kutoshiriki katika mchezo dhidi ya Man City

Kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane amethibitisha kauli hiyo

Bale hakushiriki mechi saba msimu wa 2019/2020

Gareth Bale amethibitisha kuwa hatakuwa katika timu ya Real Madrid itakayochuana dhidi ya Manchester City Ijumaa, Agosti 7.

Kwa mujibu wa jarida la UK Sun, uhusiano kati ya nyota huyo na kocha wake Zinadine Zidane umezorota kiasi kwamba hawataki kuonana uso kwa macho.

Aidha, Zinadine amefunguka kuhusu habari za mchezaji huyo kutoshiriki mchuano huo akieleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kujadiliana naye.

Real Madrid: Could Gareth Bale be Spanish club's unlikely hero ...

‘’ Nilizungumza naye moja kwa moja. Aliamua kutocheza. Mengine ni kati yangu naye, ila alisema hatacheza,’’ Zinadine.

Manchester City inakodolea macho ushindi ya ligi ya mabingwa baada ya kupoteza ligi ya premia Liverpool ikishika hatamu.

Zidane ananaonekana kuhofia uwezo wa timu yake siku chache tu baada ya kutwaa kombe la La Liga.

Kocha huyo wa Real ameweza kutwaa kombe la ligi ya Uispania mara mbili, Supercopade Espana mara mbili ligi ya mabingwa mara tatu na vile vile  UEFA mara mbili

Japo timu zote Real Madrid na Man City zina makali, kinachosalia ni kusubiri kuona mabivu na mabichi katika mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/07/pigo-kwa-real-madrid-gareth-bale-adinda-kucheza-dhidi-ya-manchester-city/

No comments:

Post a Comment