Sunday, August 9, 2020

Mo: Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja naomba wanasimba tuwe wapole

Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji maarufu kwa jina la MO amewataka mashabiki wa timu ya Simba watulie bado safari inaendelea.

“Tumetoka mbali na bado safari inaendelea tumepita mengi wanasimba wenzangu,” ameandika Dewji katika ukurasa wake wa Twitter.

“Naomba wana simba wote mtulie. Simba SC ni kubwa kuliko mtu mmoja,” aliandika Dewji.

Dewji alisema viongozi wa Simba wanafanyakazi usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bila Simba.

“Kazi inaendelea, tuko imara nguvumoja,” aliandika Twitter



source http://www.bongoleo.com/2020/08/09/mo-simba-ni-kubwa-kuliko-mtu-mmoja-naomba-wanasimba-tuwe-wapole/

No comments:

Post a Comment