Friday, August 7, 2020

Fatma: Rais Magufuli ametoa elimu bure isipokuwa anayepata mimba shuleni

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amesema ni kweli Rais John Magufuli ametoa elimu bure kwa kila mtoto.

“Isipokuwa mtoto wa kike anayeshika mimba akiwa shule,” aliandika Fatma katika ukurasa wake wa Twitter

“Kwa mtoto wa kike huyu, Magufuli anasema afukuzwe shule kabisa,” aliandika Fatma.

Fatma alisema ana swali kwa Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu akitaka kujua hao watoto wa kike wamezaliwa na wanawake au majiwe.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/08/fatma-rais-magufuli-ametoa-elimu-bure-isipokuwa-anayepata-mimba-shuleni/

No comments:

Post a Comment