Friday, August 7, 2020

Dondoo za leo; Mjumbe auwawa na wasiojulikana, Upinzani wagombana, Polisi waua wawili

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na kuuwawa kwa mjumbe, Wapinzani wagombea rangi nyekundu na mwisho ni juu ya Jeshi la Polisi kuua wawili, karibu;

WAMUUA MJUMBE

MWANZA: Wakati mchakato wa kupitisha majina ya wagombea ubunge kupitia CCM ukizidi kushika kasi, ‘watu wasiojulikana’ wanadaiwa kumteka na kumuua Mwenyekiti wa Tawi la CCM Itilabusiga- Buchosa mkoani Mwanza, IJUMAA linaripoti.

Mwenyekiti huyo aliyefahamika kwa jina la Anthony Gwalagwele, ambaye pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa CCM Kata ya Bupandwa katika jimbo la Buchosa, anadaiwa kuuawa na watu hao wakati akivua samaki katika ziwa Victoria.

Soma zaidi>>>

UPINZANI WAGOMBEA RANGI

VYAMA viwili vya upinzani nchini Uganda vimeingia katika mzozo juu ya haki ya kutumia rangi nyekundu huku kila chama kikidai kuwa kina haki ya kuitumia rangi hiyo kama utambulisho wake.

Chama kikongwe cha UPC kinadai kuwa chama kipya cha NUP kinachoongozwa na msanii maarufu kama Bobi Wine kilikosea kuanza kutumia rangi ambayo imekuwa yao kwa miaka mingi.

Lakini NUP imekanusha madai hayo ikisema imetumia rangi hiyo ikiwa vuguvugu la ‘People Power’ na hakuna aliyejitokeza kupinga hadi pale waliposajiliwa kama chama.

Soma zaidi>>>

POLISI WAUA WAWILI

JESHI la polisi mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanya operesheni maalum ya kudhibiti makosa ya jinai na kufanikiwa kuwaua majambazi wawili na kukamata silaha zao pump action na risasi kumi .

Jeshi la polisi lilipata taarifa za kiitelijensia kuwa kuna majambazi wamepanga kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha katika moja ya viwanda vilivyopo eneo la Zegereni ,Mlandizi.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/08/dondoo-za-leo-mjumbe-auwawa-na-wasiojulikana-upinzani-wagombana-polisi-waua-wawili/

No comments:

Post a Comment