Saturday, August 8, 2020

Yanga Yaibuka Baada Ya Morrison kutambulishwa Simba “Anamkataba na klabu yetu”

Morrison: Yanga SC tell forward to leave club if he 'doesn't have ...Ikiwa ni dakika chache baad aya klabu ya Simba kumtambulisha rasmi kiungo Bernard morrison kuwa mchezaji wao, klabu yake ya zamani Yanga imejibu mapigo kwa kudai kuwa unafuatilia juu swala hilo kwa kuwasiliana na shirikisho la soka nchini.

Katika barua iliyotolewa na klabu hiyo imelezwa kuwa Yanga bado wanamkataba na mchezaji huyo na wanafuatilia kwa karibu kinachoendelea mitandaoni na hatua kali zitachukuliwa kwa pande zilizohusika na swala hilo

“Uongozi unafuatilia kwa karibu na umakini mkubwa suala hilo na ikithibitika hatua kali na za mfano zitachukuliwa kwa pande zote zinazohusika,Uongozi unawataka wanachama na wapenzi wa Yanga kuwa watulivu kwani mchezaji Bernard Morrison anamkataba na klabu yetu hadi 2022” imenukuliwa barua hiyo

 

View this post on Instagram

Taarifa kwa Umma.

A post shared by Young Africans SC (@yangasc) on



source http://www.bongoleo.com/2020/08/08/yanga-yaibuka-baada-ya-morrison-kutambulishwa-simba-anamkataba-na-klabu-yetu/

No comments:

Post a Comment