Monday, August 10, 2020

UEFA Yatoa Msimamo Wake Baada ya Wachezaji Wawili Atletico Kukumbwa na Corona

championsleaguetrophyShirikisho la soka barani ulaya UEFA limethibitishwa kuwa mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya Atletico Madrid dhidi ya Leipzig utapingwa siku ya Alhamis kama ilivyopangwa awali licha ya wachezaji wawili wa Atletico kukumbwa na virusi vya corona.

Mapema jana klabu ya Atletico ikiwa njiani kulekea jiini Lisbon Ureno ilitoa taaaria kuwa wachezaji wake wawili mbao hakuwataja majina wamekutwa na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo kabla ya kuanza kwa safari hiyo.

Ilikuwa inatarajiwa kuwa mchezo huo utasogozwa mbele kutoka na majanga waliyopata atletico lakini taarifa iliyootlewa leo na UEFA imedai kuwa mchezo huo utachezwa kama ilivyopangwa awali.

Wachezaji hao wameshatengwa na hawajasafiri na timu kwenda Lisbon ambako michezo ya UEFA kwenye hatua ya robo fainali mpaka fainali itapingwa  huku fainali ikitarajiwa kufanyika Agosti 23, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/10/uefa-yatoa-msimamo-wake-baada-ya-wachezaji-wawili-atletico-kukumbwa-na-corona/

No comments:

Post a Comment