Saturday, August 1, 2020

NEC imewataka watendaji wa uchaguzi kuacha mchezo wa kufunga ofisi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimazi wote wa uchaguzi kufuata maadili na kuzingatia maelekezo waliyopewa.

Kadhalika, watendaji wa uchaguzi wametakiwa kuwepo kwenye ofisi na anayekiuka ni kinyume cha maadili na hawakubali kitendo hicho.

Akizungumza na vyama vya siasa  leo Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa mstaafu, Semistocles Kaijage, amesema tayari wameshatoa maelekezo na yanatakiwa kufuatwa.

” Tayari tumekutana na wasimamizi wote wa uchaguzi upande wa Tanzania Bara Julai 24, 2020 jijini Dodoma na msisitizo uliowekwa wazingatie maadili ya uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na NEC,”

Jaji Kaijage amesema tayari wasimamizi wa uchaguzi wameshateuliwa  na wanaendelea na mafunzo ambayo yatakamilika Jumatatu Agosti 03, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/01/nec-imewataka-watendaji-wa-uchaguzi-kuacha-mchezo-wa-kufunga-ofisi/

No comments:

Post a Comment