Saturday, August 1, 2020

Zaidi ya Sh Bilioni 300 zinatarajia kutumika katika Uchaguzi Mkuu

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa mstaafu, Semistocles Kaijage, amesema bajeti inayotarajiwa kutumika katika Uchaguzi Mkuu ni Sh bilioni 331.7.

Uchaguzi Mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 28 na kampeni zinaanza Agosti 26 hadi Oktoba 27, 2020.

Jaji Kaijage ameyasema hayo leo kwenye mkutano uliowakutanisha vyama vyote vya siasa nchini.

Aidha, amesema daftari la wapiga kura lina idadi ya wapigakura 29,188,347.

Jaji Kaijage alifafanua kuwa kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/01/zaidi-ya-sh-bilioni-300-zinatarajia-kutumika-katika-uchaguzi-mkuu/

No comments:

Post a Comment