Tuesday, August 4, 2020

Mikel Arteta Awataja wachezaji 9 Anaowauza Kujipanga kwa Msimu Ujao Baada ya Kutwaa FA

How the PL table would look if it began when Arsenal appointed Arteta

Arteta ana mpango wa kupata fedha za kuwasaini wachezaji wapya wenye makali zaidi. Picha: Hisani

Arteta ana mpango wa kuwauza zaidi ya wachezaji tisa kabla ya  msimu ujao

Hii ni baada ya Arsenal kutwaa kombe la FA kwa kuicharaza Chelsea 2-1, Wembley

Kocha huyo ana mpango wa kupata fedha za kuwasaini wachezaji wapya wenye makali zaidi

Mikel Arteta ana mipango kadha wa kadha na klabu yake ya Arsenal, hii ni baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya FA na kupiku Chelsea kwa mabao 2-1.

Meneja huyo aliyemridhi Unai Emery katika klabu hiyo miezi nane iliyopita amepata fahari kubwa sasa akiwa katika orodha ya mameneja walioweza kutwaa taji.

Ushindi wao katika FA sasa unaipa klabu hiyo nafasi ya kushiriki katika ligi ya Uropa msimu ujao, Arteta akianza kujipanga na mapema.

Kulingana na ripoti ya SunSports, Arteta ana mpango wa kuwauza zaidi ya wachezaji wake tisa kama njia ya kupata fedha za kuipanga vyema timu yake kwa wachezaji wenye ujuzi zaidi.

Jarida hilo limebaini kuwa bajeti ya Arteta imepanda kwa £30 milioni baada ya kutwaa ligi ya FA kwa kuipa adabu Chelsea.

Aidha, chapisho hilo limebaini kuwa wachezaji watatu kati ya timu iliyopiga Chelsea wapo kwenye orodha ya mauzo.

Alexandre Lacazette anadaiwa kuongoza katika orodha hiyo ya wachezaji wanaogura Arsenal.

Wengine wanaodaiwa kupasha misuli moto tayari kuondoka ni pamoja na Shkodran Mustafi, Sead Kolasinac, Sokratis Papastathopoulos, Lucas Torreira, Henrikh Mkhitaryan, Matteo Guendouzi na Mesut



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/mikel-arteta-awataja-wachezaji-9-anaowauza-kujipanga-kwa-msimu-ujao-baada-ya-kutwaa-fa/

No comments:

Post a Comment