Tuesday, August 4, 2020

Covid19: Maafisa wa Afya Walazimika kuufukua Mwili Usiku Kwa Hali ya Kutatanisha

Family and friends gather for the burial of Kenya’s first medic victim of Covid-19 Dr Doreen Adisa Lugaliki at Ndalu village, Tongaren sub-county in Bungoma County.

Mazishi daktari aliyefariki na Covid19. Picha:Hisani

Mafisa hao wa afya wanaohusika na maziko ya waliofariki na virusi vya corona walilazimika kuufukua mwili mmoja eneo la Shamakhokho baada ya kuuzika mwili usiofaa.

Maafisa hao waliuzika mwili mwingine badala ya Linus Simwa, pasta ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya Vihiga aliyefariki kutokana na virusi vya corona.

Wahudumu katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti waliweza kugundua mchanganyiko huo baada ya jamaa kukujia maiti wao na kuukosa chumbani humo.

Walishangaa kuona kuwa mwili wa Linus Simwa waliojua kuwa tayari ulichukuliwa ulikuwa mle ndani.

Hapo wakalazimika kuufuata ule mwingine hadi alikozikwa ili kuufukua na kupewa kwa wenyewe kwa maziko.

A medical practitioner dressed in protective gear at Coronavirus isolation and treatment facility in Mbagathi District Hospital on Friday, March 6, 2020.

Mhudumu wa afya akivalia magwanda ya kujizuia na corona. Picha: Hisani

‘’ Matambiko kadha wa kadha yalizimika kufanyika maana hatukujua tuliyemzika hapa,’’ Modlyn Imbayi, Chifu wa Shamkhokho alisema.

Simwa alifariki Jumatano, Julia 29 katika hospitali ya rufaa ya Vihiga baada ya kuugua kwa wiki huku jamaa huyo mwengine akifari muda mfupi tu baada ya kulazwa hospitalini humo.

Wawili hao walitiwa katika mifuko ya maiti na kuwekwa makavazini suala ambalo linakisiwa kuibua mchanyiko huo.

Maiti ya wnaofariki na covid hawarus kuonekana na jamaa, n maafisa wa afaya ndio wanaoruhusiwa kuuzika, hii huweza kuchangia mchanganyiko mkubwa zaidi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/covid19-maafisa-wa-afya-walazimika-kuufukua-mwili-usiku-kwa-hali-ya-kutatanisha/

No comments:

Post a Comment