Friday, August 7, 2020

Membe atinga Dodoma kuchukua fomu ya kugombea urais

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amekwenda kuchukua fomu ya kugombea urais jijini Dodoma.

Membe amewasili mapema kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad Sharif.

Kiongozi huyo hivi karibuni alijiunga na Chama cha ACT-Wazalendo na kuteuliwa kwenye kura za maoni kugombea urais kupitia chama hicho.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/07/membe-atinga-dodoma-kuchukua-fomu-ya-kugombea-urais/

No comments:

Post a Comment