Monday, August 10, 2020

Lissu Afanya Misa Ya Shukran Singida Ahaidi Mazito

Image

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amefanya misa ya shukrani kwenye jimbo alilowahi kulingoza kwa miaka kadhaa  Singida Mshariki baada ya kufika jimboni hapo leo kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 3.

Lissu amefanya misa hiyo leo Agosti 10, 2020 Kwenye Kanisa la parokia ya Mtakatifu Ritta Wakashia lililopo Ikungi kwenye jimbo hilo alilolingoza ka takribani miaka 10 akiwa na chama cha CHADEMA na kuhaidi kuwa hata lipa kisasi kwa watu wote ambao walisababisha apate maumivu.

“Naahidi sitampitisha mtu yeyote kwenye maumivu yale niliyoyapata hata kama atakuwa amenikosea kwa kiwango gani…” amesema Lissu wakati wa misa hiyo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/10/lissu-afanya-misa-ya-shukran-singida-ahaidi-mazito/

No comments:

Post a Comment