Monday, August 10, 2020

Polisi Wampiga Risasi Jamaa Aliyepatikana Akipalilia Mimea ya Bangi Shambani

2019: Bangi itahalalishwa Kenya mwaka huu? – Taifa Leo

Mmea wa bangi. Picha:Hisani

Polisi walikuwa wakimsaka jamaa huyo ambaye alishirikiana na wenzake kumshambulia mmoja kwa panga

Polisi walienda hadi nyumbani kwake walikojificha washukiwa hao

Mwanawe alifichua kwa polisi hao kuwa babake alikuwa shambani licha ya mkewe kukataa

Maafisa wa polisi wa kituo cha Hindi walikuwa na  kibarua kigumu katika kuwakamata washukiwa waliomshambilia kinyama mwezao kwa panga kisha kutoroka.

Katika kisa hicho kilichofanyika Jumapili, Agosti 9, maafisa hao walilazimka kuelekea hadi katika kijiji cha Sasi walikoishi washukiwa hao kwa lengo la kuwakamata.

Wakiongozwa na Sammy Kamwara, maafisa hao walifanikiwa kufika katika boma la Rasta, jamaa aliyekuwa akiishi na washukiwa hao nyumbani kwake.

Walipowasili humo, mkewe rasta aliwaambia maafisa hao kuwa mumewe hakuwepo, hata hivyo mwanao mdogo alimwaga mtama akieleza kuwa babake alikuwa kondeni akipalilia nyuma ya nyumba tu.

Mbunge wa Geita ataka bangi, mirungi vihalalishwe | East Africa ...

Ukulima na uvutaji wa bangi ni marufuku Tanzania. Picha: Hisani

Maafisa hao walifululiza hadi shambani humo na kumpata Rasta akiipalilia mimea ya bangi akiwa na wenzake.

Wengine hao wote walitoroka mbio kuwahepa maafisa wa polisi huku Rasta akibaki tayari kukabiliana nao uso kwa macho.

Rasta alichukua panga yake na kutishia kuwavamia maafisa hao lakini wakampiga risasi mara kadhaa kabla kufikiwa na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Bangi ni mmea ambao umepigwa marufuku nchini Tanzania.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/10/polisi-wampiga-risasi-jamaa-aliyepatikana-akipalilia-mimea-ya-bangi-shambani/

No comments:

Post a Comment