Monday, August 10, 2020

Fatma Karume Acharuka “Mkapa Aliua Tume Sio Huru”

FATMA KARUME AKOLEZA JOTO UCHAGUZI TLS - Mtanzania

Aliyekuwa Rais wa chama cha wanasheria cha Tanganyika (TLS) Fatma Karume amesema Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania  hayati Benjamin Mkapa alijua kuwa tume ya uchaguzi hakikuwa huru ndio maan alisimamana kudai tume huru akiwa hai.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na mtangazaji wa muda mrefu Salama Jabir, amesema kuwa tume ya sasa haipo huru kwakua wapo watendaji wa tume hiyo wanaofanya kazi kwa kuteuliwa na rais wa Tanzania aliyopo madarakani kinyume na matakwa ya katiba.

“Mkapa alikuwa anasiama na kusema tunahitaji tume huru ya uchaguzi sababu alikuwa anajua tume ya uchaguzi ilianza kubamwa kisheria kwenye uongozi wake ndio maan alisimama bila aibu na kudai kupata tume huru ya uchaguzi” amesema Fatma Karume.

Fatma Karume ni mmoja kati ya waanziilishi wa kampeni ya kudai tume huru ya uchaguzi mtandaoni kwa kuvaa nguo nyeupe mpaka siku ya kupiga kura ili kuwakumbusha wananchi juu ya uwepo wa tume.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/10/fatma-karume-acharuka-mkapa-aliua-tume-sio-huru/

No comments:

Post a Comment