Sunday, August 9, 2020

Dondoo za leo; Marekani yaonya raia wake kutembelea hapa, Mama atiwa mimba na mwanae na Simba yambana Senzo

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja Marekani yaonya raia wake kutembelea Kenya, Mama atiwa mimba na mwanae na mwisho ni juu ya Simba kumbana Senzo.

Karibu;

MAREKANI YAONYA RAIA WAKE KUTEMBELEA KENYA

Taifa la Marekani ambalo kwa sasa ndio kitovu cha COVID-19, limetoa tahadhari kwa raia wake dhidi ya kusafiri Kenya kutokana na kuongezeka maradufu kwa visa vya COVID-19.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC) kiliwashauri raia wake kufuta usafiri wao mintarafu ya serikali ya Kenya kulegeza baadhi ya masharti ya kukabili COVID-19 na hivyo kuwa hatari kwa raia wake.

Soma zaidi>>>

ATIWA MIMBA NA MWANAE

Mama wa miaka 40, Betty Mbereko wa huko nchini Zimbabwe anataka aoelewe na mtoto wake wa kiume Farai Mbereko (23). Imeelezwa kuwa wawili hao wako kwenye mapenzi makali na hivyo kuamua kuupeleka uhusiano wao kwenye level nyingine ya ndoa huku tayari mama huyo akiwa na ujauzito wa miezi sita aliopewa na mwanae.

Embu tuambie, unadhani dunia inaelekea wapi?

Soma zaidi>>>

SIMBA YAMBANA SENZO

UONGOZI wa klabu ya Simba umeeleza kushtushwa na taarifa ya kujiuzulu kwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa ambaye anahusishwa na kujiunga na Yanga.

Barua ya klabu hiyo iliyowekwa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii leo Agosti 9, 2020 imeeleza kuwa Simba haitahusika na jambo lolote linalohusiana na Senzo atakalolifanya kuanzia sasa.

Simba imemtaka ajieleze kuhusu mambo ambayo hayajakamilika na kufanya makabidhiano kwa weledi na haraka iwezekanavyo.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangazie jambo hili la mdau anayeomba ushauri jinsi ya kuishi na Boyfriend wake mchafu;

Kuna mdau anaomba msaada wa namna ya kuishi na Mwanaume yaani ‘Boyfriend’ wake asiye na tabia ya usafi kuanzia mwilini hadi mahali anapokaa (ndani kwake)

Mdau anasema “Mimi sio mtu msafi sana ila Mwanaume huyu amenishinda. Ni mtu mzuri na nimekuwa naye kwa miezi 8 sasa, mwanzo sikuwa nimemuelewa ila huyu Mwanaume ni mchafu sana.”

Anaendelea “Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi. Yaani analala na Mwanamke usiku, asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Hata nikisema hasikii wala haelewi, ndio kwanza anasema nampanda kichwani.”

Aidha, amesema “Chumba chake ndo kichafu usiseme. Kuna wakati nilisafiri kama mwezi hivi kurudi chumba hakitamaniki. Nikamsafishia na kila weekend nikawa naenda kusafisha. Nilipata ugeni na sikwenda kwake kama wiki mbili, nilivyoenda nilikuta sahani alizolia chakula siku kama 3 zilizopita zipo humo, machupa ya maji, maganda ya ndizi”

Mdau anaomba maoni yenu amfanye nini boyfriend wake aache hiyo tabia na je, anaweza kuishi naye vipi?



source http://www.bongoleo.com/2020/08/10/dondoo-za-leo-marekani-yaonya-raia-wake-kutembelea-hapa-mama-atiwa-mimba-na-mwanae-na-simba-yambana-senzo/

No comments:

Post a Comment