Tuesday, August 4, 2020

Msajili Awaonya CHADEMA


Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi ameionya CHADEMA kutokana na alichokiita uvunjifu wa sheria kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa Taifa

Alizungumza leo Jaji Mutungi amesema kitendo hicho kilifanywa jana wakati Baraza Kuu la CHADEMA lilipokuwa likimpendekeza atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais.

“Nimesikitishwa na kitendo cha kuvunja sheria kwa makusudi kilichofanywa na CHADEMA cha kuchukua wimbo wa Taifa na kuongeza aya Kwa hili ambalo limefanywa na CHADEMA ni kama kunajisi wimbo wa taifa, Nataka kuwaonya wakati wanaendelea na mikutano yao, waheshimu sheria za nchi” amesema Jaji Mutungi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/msajili-awaonya-chadema/

No comments:

Post a Comment