Tuesday, August 4, 2020

Mbowe: Tupo Tayari Kushirikiana Kwa Ajili Ya Kutuhimarisha


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema chama hicho kipo tayari kushirikiana na chochote cha siasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaendeleaje kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City amesema watashirikina kwa lengo la kuongezea nguvu chama hicho na si tofauti na hivyo.

“Tuko tayari kuishiriki dhana ya ushirikiano, lakini ushirikiano usiotupunguza ktk nguvu ya malengo yetu, tukikubali kushirikiana na wenzetu siyo kwamba tumekosa wagombea ila ni kwa sababu tunaamini pengine wenzetu wana mgombea bora zaidi”amesema Mbowe.

Kwa kipindi cha hivi karibuni washauri wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakitoa ushauri kwa vyama vya upinzani kuungana kwa ajili ya kuviimarisha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/mbowe-tupo-tayari-kushirikiana-kwa-ajili-ya-kutuhimarisha/

No comments:

Post a Comment