Tuesday, August 4, 2020

Mbowe Atuma Ujumbe Kwa Magufuli “Umetusaidia”


Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema chama hicho kina mtumia Rais John Magufuli kama fursa ya kutoa wanachama upupu ndani ya chama hicho.

Akizungumza leo wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaendelea jijini Dar es salam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

“Na sio kweli kuwa Magufuli ni hatari wakati wote, wakati mwingine amekuwa ni fursa kwetu, ametusaidia kutuondolea ule upupu uliobakia kwenye Chama chetu” amesema Mbowe.

Baadhi ya wananchama waliokiama chama hicho na kukimbilia chama cha Mapinduzi (CCM) waliangukia pua kwenye kura za maoni za kuwania ubunge kwenye chama hicho.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/mbowe-atuma-ujumbe-kwa-magufuli-umetusaidia/

No comments:

Post a Comment