Tuesday, August 4, 2020

Maalim Seif Atuma ujumbe CHADEMA.

ImageMwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo  Maalim Seif Sharif Hamad ametoa wito kwa vyama vya upinzani nchini kuhakikisha wanajipanga kupigania ushindi kwakua tume haitatenda haki.

Akizungumza kwenye  mkutano mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) unaoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mlimani City.

“Wito wangu kwenu tujipange, tusitegemee kama tume itatenda haki, tujipange kisawasawa kuhakikisha endapo tutashinda, Hakuna na asiwepo wa kuzuia ushindi wetu” amesema Maliim.

Chama cha demokrasia na maendeleo kinaendela na mkutano mkuu wa chama hichio wenye lengo la kupitisha mgombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/maalim-seif-atuma-ujumbe-chadema/

No comments:

Post a Comment