Saturday, July 11, 2020

Zitto: Watanzania bado ni masikini kutamba na uchumi wa kati ni kuwatukana watu

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Watanzania bado ni masikini katika nchi yenye kila aina ya utajiri.

Zitto amesema ukitazama mkoa wa Rukwa nusu ya watu ni masikini wa mahitaji ya msingi.

Zitto ambaye alikuwa Mbunge wa Kigoma Mjini aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter.

“Hawana uwezo wa kutumia hata shs 1500 kwa siku. Kutamba na uchumi wa kati ni kutukana watu,” aliandika Zitto.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/12/zitto-watanzania-bado-ni-masikini-kutamba-na-uchumi-wa-kati-ni-kuwatukana-watu/

No comments:

Post a Comment