Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba ni Rais John Magufuli amtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha TIC, Ni Simba Vs Yanga leo nani kuchukua ushindi? na Sheikh Ponda akamatwa kulikoni?
Karibu msomaji wetu;
Rais Magufuli Atumbua Kigogo TIC
Rais John Magufuli leo amemteua Dk. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Kazi alikuwa Meneja wa Idara ya Sera za kibajeti na madeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imeekeza kuwa Dk. Kazi anachukua nafasi ya Godfrey Idelphonce Mwambe.
Ni Simba Vs Yanga
Leo Julai 12, 2020 ni siku ya kukumbukwa kwenye macho ya wapenda soka nchini na nje ya nchi kutokana na mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la shirikisho la Azam, mchezo huu unakuwa wa aina yake kwakua unawakutanisha maasim wawili.
Ni Simba Vs Yanga timu zilizokutana takribai mara 99 mpaka kufikia mwaka 2019 huku rekodi ziibeba yanga kutokana na kufanikiwa kushinda takribani michezo 38 huku Simba wakiwa wameshinda mara 28 na wakiwa wametoka sare mara 35.
Sheikh Ponda Akamatwa
Katibu wa jumuhi ya za Waislam nchini Shiekh Issa Ponda amekamatwa ns jeshi la polisi kwa mahojiano juu ya walaka wa uchochezi aliolitoa hivi katibuni.
Akizungumza baada ya kuthibitisha kumkamata katibu huyo, Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema wamemkamata baada ya kuona andiko hilo.
“Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa Mahojiano ya Uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita Waraka. Tunamhoji kutokana na ule Waraka, Yeye kakubali kwamba ni wake na Taasisi yake lakini Viongozi wote wa Taasisi wameukana”amesema.
No comments:
Post a Comment