Sunday, July 12, 2020

Fatma Karume ampasha Dk Mwinyi kuwa Wazanzibari hawawezi ubabe wala ukali

Wakili wa Kujitegemea, Fatma Karume amesema Dk. Hussein Mwinyi anataka kuiendesha Zanzibar kwa ukali jambo ambalo wazanzibari hawajalizoea.

“Hussein anataka kuiendesha#Zanzibar kwa ukali,” Fatma aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter akijibu kile ambacho Dk. Mwinyi amekieleza

Dk Mwinyi alisema akiwa Rais Zanzibar atatumia staili ya Magufuli kuongoza Zanzibar.

Fatma aliandika kuwa “Wamarekank wanamsemo kwenye mchezo wa Baseball Strike one. Tukutane oktoba 2020 maana wazanzibari hatuwezi ubabe na ukali hata chembe. Ajifunze kuwa Mardhia,”.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/12/fatma-karume-ampasha-dk-mwinyi-kuwa-wazanzibari-hawawezi-ubabe-wala-ukali/

No comments:

Post a Comment