Monday, July 20, 2020

Zitto Kabwe Atema Cheche “Hatutasusia Uchaguzi”

Zitto kabwe asema yuko tayari kuwajibika – Dar24Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema vyama vya upinznai nchini havitasusia uchaguzi mkuu ujao kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mapema mwaka 2019.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa muda mrefu Jenerali Ulimwengu nyumbani kwake mjini Dar es salaam,Zitto amesema wanafahamu kuwa tume haiko huru na hata mazingira hayako sawa lakini hawatofanya kosa hilo.

“Tunajua kabisa mazingira hayako sawa na tunajua kabisa tume haiko huru lakini hatuwezi kususia kugombea uchaguzi kwakua tunaomba haki huku tunagombea ili kuhakikisha hali yetu ya msingi inalindwa na tume ya uchaguzi” amesema Zitto.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka 2019 vyama vyote vya upinzani vilisusia uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni kutoka na wasiamizi wa uchaguzi huo kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni makada wa wazi wazi wa chama cha mapinduzi (CCM).

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/zitto-kabwe-atema-cheche-hatutasusia-uchaguzi/

No comments:

Post a Comment