Monday, July 20, 2020

Wananchi Waandamana London Kupinga Uvaaji wa Barakoa

Maandamano hayo yalipangwa na kundi moja ndogo la ‘Keep Britain Clean’. Picha: Hisani

Mamia ya waandamani walijazana katika barabara za mji wa London kupinga vikali hatua iliyochukuliwa na serikali kutangaza uvaaji wa barakoa kuwa lazima.

Waziri Mkuu Boris Johnson alitangaza Ijumaa, Julai 17 kuwa uvaaji wa barakoa utakuwa lazima haswa katika maduka ya jumla na katika maeneo ya umma.

Tangazo hili liliwakwaza baadhi ya wakazi wa mji huo waliojitokeza kuandamana kupinga vikali hatua hiyo wakiitaja kama njia ya kujaribu kudhibiti akili za watu.

Maandamano hayo yalipangwa na kundi moja ndogo la ‘Keep Britain Clean’ ambalo linasimamia Uhuru wa mazungumzo, maamuzi na fikra.

Hundreds attended the rally in Hyde Park.

Waziri Mkuu Boris Johnson alitangaza Ijumaa, Julai 17 kuwa uvaaji wa barakoa utakuwa lazima. Picha: Hisani

Tafiti kadhaa zimebaini kuwa virusi vya corona huweza kusambaa kupitia kwa hewa na hivyo njia ya kipekee ya kuweza kuvizuia ni kuvalia barakoa.

Licha ya hayo, utafiti uliofanywa hivi majuzi umebaini kuwa 25% pekee ya Waingereza ndio wanaovalia barakoa katika maeneo ya umma ikilinganishwa nchi zingine kama Italia ambako zaidi ya 83% huvalia barakoa hizo.

Waziri Mkuu Johnson ameeleza kuwa uvaaji wa barakoa utakuwa lazima kwa maduka ya jumla na yeyote atakayepatikana kukaidi kanuni hiyo atatozwa faini ya $125.

Boris alionekana akivalia barakoa juma lilopita licha ya serikli yake kupinga vikali umuhimu wa barakoa hizo awali.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/wananchi-waandamana-london-kupinga-uvaaji-wa-barakoa/

No comments:

Post a Comment