Thursday, July 16, 2020

Zindzi  Mandela Alipatikana na  Covid19, Mwanawe Afunguka

Zimbio.

Zindzi  Mandelau alifariki katika mkoa wa Gauteng, eneo lilotajwa kama ngome ya virusi  vya corona Afrika Kusini. Picha: Hisani.

Zondwa Mandela alisema kuwa mamake alithibitishwa kuambukizwa viusi vya corona siku aliyoaga dunia.

Hata hivyo alisema kuwa virusi hivyo sivyo vilivyosababisha kifo cha mamake.

Mama huyo mashuhuru alifariki katika mkoa wa Gauteng, eneo lilotajwa kama ngome ya virusi hivyo hatari Afrika Kusini.

Zindzi Mandela, mwanawe aliyekuwa rais maarufu wa Afrika Kusini Nelson Mandela alipatikana na virusi vya corona siku aliyofariki.

Hata hivyo mwanawe Zindzi, Zondwa Mandela amekanusha uwezekano wa mamake kufariki kutokana na virusi hivyo.

‘’Hata hivyo, kupatika na virusi hivyo haimaanishi kuwa alifariki kutokana na navyo. Maana alipatikana na virusi hivyo, tunanahitajika kufuata kanuni zifaazo,’’ Aliliambia SADC Jumatano, Julai 15.

Familia ya Mandela ilithibitisha kuhusu kifo cha mama huyo mashuhuru mwenye umri wa miaka 59 Jumatatu, Julai 13 katika hospitali ya Johannesburg, mkoa wa Gauteng, eneo lililotajwa kama ngome kuu ya virusi vya corona nchini humo.

Zindzi alihudumu kama balozi wa nchi ya Afrika Kusini nchini Denmark kabla kifo chake.

Alipata umaarufu mkubwa 1985 haswa baada ya kuisoma hotuba ya babake ambako alikataa kabisa ofa ya uhuru kutoka kwa aliyekuwa rais kwa wakati huo Pieter Willem Botha kutokana na uongozi wa unyanyasaji.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/zindzi-mandela-alipatikana-na-covid19-mwanawe-afunguka/

No comments:

Post a Comment